Social Icons



Jumapili, 2 Agosti 2015

FID Q AIKATAA SIASA KWA KUOGOPA UONGO WAKE.



Star na mkali wa muziki wa Hip Hop Africa Farid Kubanda a.k.a Fid Q ameeleza kuwa hana mpango wowote wa kuingia katika siasa za kibongo licha ya kuombwa na watu wengi kugombea nafasi yoyote katika siasa.

Maelezo hayo ameyaongea baada ya kuonekana wimbi kubwa la wasanii
wengi kugombea nafasi mbalimbali na wengine kutemwa na baadhi kupata ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama vyao.

Alipoulizwa alinena haya....

>>>Sijioni kuwa Mwanasiasa ingawa takribani miaka 4 iliyopita na kila siku nakutana na watu wananiambia kuwa nafaa kuwa Mwanasiasa kutokana na uwezo wangu wa kuchanganua mamb>>>

>>>Kinachonishinda kwenye siasa kuna siku nilijifunza mapinduzi ni kitu kinachoendelea,tunakaa mtaani tunaimba Malaria mara inakuja Dengue,tunaimba kuhusu mafuriko mara yanakuja mabomu na serikalini kupo hivyo unaingia ndani unakuta kuna mapengo kibao kwa hiyo utaamua mwenyewe kama utakua mkweli au lah na ukitaka kuwa mjuaji sana kuna matatizo yake pia>>>

>>>Nachokiogopa ni kuwa Mwanasiasa nipate zile hela nyingi halafu nianze kuwa wa uongo hicho ndicho kinachonitisha lakini sioni kama siasa inanishinda naogopa uongo wa siasa>>> Fid Q

Hakuna maoni:

FOOTBALL NEWS

 
Blogger Templates