Ukubwa wa hit singo za wasanii wa Tanzania huwa zinabadilisha vitu vingi sana ukiachana na vile vinavyoonekana moja kwa moja vipo ambavyo pengine mpaka upate nafasi ya kuviuliza ndipo ufahamu.
Shetta mkali kwenye game ya Bongo Fleva kwenye Exclusive interview
na Millard Ayo amesema singo ya Shikorobo peke yake imemfanya baadhi ya vitu kushindwa kuvifanya.
Ameanza kwa kusema>>> Kwa
mtu anayemtaka Shetta kwa sasa inabidi akubaliane na timu yangu ya watu
10 nina mpiga picha, nina security, Manager na Dancers na nina mtu wa
kuimba naye jukwaani (back vocal)>>>
Pia aliongeza kwa kusema >> ‘kwa sasa sisafiri tena na basi na kwa zile sehemu ambazo hakuna ndege mara nyingi huwa nauliza namna ya kupata usafiri binafsi>>>
Mengine amesema hata bei ya show zake kwa sasa zimepanda >>> Watu wamemzoea Shetta wa Milion 3 au 4 sasa hivi nachaji kuanzia dolar 5,000 (zaidi ya Milion 10 za Kitanzania kwa sasa). >>>> Shetta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni