Baada ya kuzuiliwa kutoka nchini Ufilipino kwa siku mbili hatimaye Chris Brown kaachiwa huru na kuondoka salama kabisa… msanii huyo ambaye alikuwa mjini Manila kwa ajili ya show alizuiliwa kuondoka siku ya Jumatano kutokana na madai ya kuwa hakutimiza wajibu wake wa kimkataba kipindi cha Mwaka mpya kuingia 2015.
Licha ya kuachiwa huru Chris Brown
alichukua time na kupost Twitter kusema hakuhusika na madai hayo na
alitimiza wajibu wake wa kimkataba kwani alirudi kutoa show nyingine
kufidia show aliyoikosa mwaka mpya.
>>> “Manila
mmetisha sana, nawapenda sana…ishu iliyotokea sio ndogo na aliyehusika
kufanya hivi inabidi atafutwe, jina langu limetumika na sikufanya
CHOCHOTE!!”<<< Chris Brown.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni