Snoop Dogg
Kusikia Rapper Snoop Dogg kukamatwa na Polisi kisa dawa za kulevya sio story mpya kabisa, stori ni kwamba jamaa alipokuwa
kwenye show Sweden, baada ya kumaliza alikamatwa na Polisi wakati
akiwa anajiandaa kurudi zake Marekani.
Snoop
alikamatwa akihusishwa na kosa la kutumia dawa za kulevya
kitu ambacho
ni kinyume cha Sheria za Sweden… baada ya kumfanyia vipimo vya Uchunguzi
walimwachia baada ya vipimo kuonesha jamaa hakuwa ametumia dawa hizo.
Kiukweli jamaa alikasirishwa sana na hii
ishu na anaona kama Polisi walionesha vitendo vya Kibaguzi kumkamata,
baada ya hapo jamaa kaapa kwamba hatamani hata kidogo kurudi tena Sweden
>>>> “Samahani sana mashabiki
wangu wote wa Sweden, sitorudi tena kwenye nchi hii… Mtamshukuru Bosi
wenu wa Polisi na wahusika wote wa Idara ya Polisi ila ndio nshamaliza” >>>> Snoop Dogg.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni